Sunday, November 23, 2014

KWA VIONGOZI WA CONFERENCE, KANDA , MATAWI NA WANACHAMA WOTE;

YAH: UTARATIBU MPYA WA KULIPIA KIINGILIO KWA WALIOCHELEWA.

Wapendwa salaam! Baada ya deadline ya STU na bado maombi yetu ya kuongezewa muda kutojibiwa mpaka sasa,  tulifanya mawasiliano na uongozi wa NTUC( Nothern Tanzania Union Conference) kuhusu kulipia maana wao wamepewa mpaka trh 30/11/2014.
Tuliwaomba kuwa wanachama wetu walipie  kupitia kwao, Mungu ni mwema walitukubalia. Kutokana na hilo tunawatangazia utaratibu ufuatao.

1. Malipo yote yafanyike katika, TANZANIA UNION OF SDA CHURCH. Account number ; 014105000721 NBC BANK,

2.Tarehe ya mwisho ya kulipia ni 30/11/2014.

3.Baada ya malipo PAY IN SLIP zote ziscaniwe na kutumwa kwa uongozi wa TUCASA-STU. Zitumwe kwa kupitia kamati zilizowekwa kwa ajili ya retreat hiyo. Ni matumaini yangu kuwa kila kanda ina kiongozi anaehusika na jambo hilo.

4. Baada ya watu kulipia watajisali online kupitia: bit.ly/ecdyouthretreat2014.
hii ni kwa sababu NTUC hawajaweka utaratibu wa receipt number tofauti na sisi ambapo mtu hutakiwa kupata receipt number yakekwa ajili ya kujisajilia. Kwa hiyo katika kujisajili sehemu inayohusu Union unayotokea andika NOTHERN TANZANIA UNION CONFERENCE(NTUC).

5. Kumbuka kwa wote waliolipia na watakaolipia kubeba PAY IN SLIP ZAO kipindi tutakapoenda Kenya. Mjulishe  na mwenzako.

Wenu katika utumishi shambani mwa Bwana.
  Maliwanga Basilio .R. (Mhazini TUCASA-STU)
Posted by Unknown on 12:58 PM  No comments »

Sunday, November 16, 2014




Posted by Unknown on 11:47 AM  No comments »

Tuesday, November 11, 2014





Posted by Unknown on 1:55 PM  1 comment »
Ndugu kiongozi, napenda kukumbusha kujiandaa na kikao cha kanda (Darzone EXCOM) kitakachofanyika katika kanisa la waadventista wa Sabato mwenge jumapili  (16/11/2014). Aidha kwa upande wa agenda tunazotegemea kuwa nazo ni pamoja na
1.  UFUNGUZI WA KIKAO.
2 .TAARIFA YA KIKAO KILICHOPITA.
3 .MIPANGO YA UINJISTI.
4. TAARIFA ZA CHAMA NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA VIONGOZI.
5 .RATIBA YA MATUKIO MUHIMU.
6. TAARIFA ZA MUHIMU KUTOKA KWA VIONGOZI MFANO MATUKIO YALIYOJIRI KAMA RETREAT, REBEKA FUND ....
7 .MENGINEYO
8.  KUFUNGA KIKAO.
NB. Kwa wanachama mnakumbushwa kuombea kikao hiki ili maamuzi na mipango inayoafikiwa iongozwe na Roho wa Mungu.
Karibuni sana na Mungu awabariki.
Posted by Unknown on 1:24 PM  No comments »



Posted by Unknown on 12:56 PM  No comments »

Bookmark Us

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter

Search